Ziara ya maeneo yaliyoibuliwa katika mradi wa Scale

Ziara ya kamati ya mradi wa kuibua vipaumbele vinavyotokana na mabadiliko ya Tabianchi (SCALE) kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati kutoka Baraza la Manispaa Magharibi ‘A’ wakutembelea katika maeneo (Mwera , Kama na Welezo) yaliyoibuliwa kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa mradi ambao unatekelezwa na World Bank.

Mikakati ya usafi kwa Mkoa Mjini Magharibi

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Moh’d Ali Abdalla amevitaka vikundi vinanyosimamia usafi wa mji katika Wilaya ya Magharibi ‘A’ kuongeza kasi ya utendaji kazi ili lengo la utunzaji na uimarishaji wa mji uweze kufikiwa kwa ufanisi Zaidi .
Ameyasema hayo alipokutana na vikundi hivyo vinanyosimamia shuhuli za ukusanyaji wa taka katika shehia mbali mbali zilizomo ndani ya Wilaya hiyo.

Ziara ya Kamati ya Fedha

Kamati ya Fedha na Mipango ya Baraza la Manispaa Magharibi ‘A’ ikiongezwa na Mstahiki Meya wa Baraza Mh. Chum Shuwar Machano, ikitembelea maeneo ya vyanzo vya mapato na maeneo yanayomilikiwa na Baraza la Manispaa Magharibi ‘A’.