


TIMU ya kushughulikia Mradi wa SCALE kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za (SMZ), imetoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Kamati za Kushughulikia Malalamiko za Wadi, kwa lengo la kuwajengea uwezo katika mfumo wa kushughulikia malalamiko, afya na usalama katika maeneo ya kazi.
