Divisheni

DIVISHENI ZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA ZILIZOIDHINISHWA NA SERIKALI

Baraza la Manispaa ya Magharibi “A” lina divisheni tatu (3) nazo ni:-

1) Divisheni ya mipango, utumishi na utawala.

2) Divisheni ya mazingira na mipango miji.

3) Divisheni ya mapato, uchumi na ujasiriamali.

Divisheni hii itahusika na kusimamia masuala yote ya Kiutumishi na utawala ikiwemo ajira, maendeleo ya watumishi, kupanda vyeo, kutetea haki na maslahi ya watumishi na mwajiri pamoja na masuala ya kibinaadamu kwa watumishi.

Divisheni hii ina Sehemu nne (4) ambazo ni Sehemu ya Utumishi, Sehemu ya Utawala, Sehemu ya Mipango  na Sehemu ya Utunzaji kumbukumbu.

Majukumu ya divisheni ya mipango utumishi na utawala

1. Kutoa ushauri wa kujaza nafasi zinazohitaji watumishi kujazwa.

2. Kuratibu tathmini ya mahitaji ya ujengaji uwezo na mafunzo, kuainisha mapungufu ya uwezo uliopo na kubaini fursa za maendeleo kwa watumishi.

3. Kutoa msaada wa ushauri nasaha kwa watumishi wenye vikwazo mbali
mbali katika utendaji.

4. Kuratibu uthibitisho kazini, upandishwaji vyeo, uhamisho, kuacha kazi,
malalamiko na masuala ya nidhamu kwa mujibu wa taratibu.

5. Kutunza kumbu kumbu sahihi za watumishi wote.

6. Kukusanya takwimu na kumbu kumbu zote zinazohusu mipango ya
watumishi.

7. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na
mwaka.

8. Kuweka kumbu kumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi.

9. Kusaidia kusimamia nidhamu ya wafanyakazi.

10. Kuainisha matatizo ya wafanyakazi.

11. Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya Ofisi ikiwemo vyombo vya
usafiri, magari, samani, (Road Furniture vifaa vya kuandikia na vifaa vya
mawasiliano.

12. Kusimamia majengo na mali nyengine zisizohamishika.

13. Kuratibu na kushughulikia masuala mtambuka ndani ya taasisi.

Divisheni hii itakuwa na jukumu la kusimamia na kutoa huduma ya usafi na usimamizi wa taka ngumu, maji taka na mazingira katika maeneo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Divisheni hii ina sehemu tatu (3)  ambazo ni Sehemu ya Mazingira, Sehemu ya Mipango Miji na Sehemu ya Uimarishaji Miundombinu.

Majukumu ya divisheni ya mazingira na mipango miji

1. Kusimamia masuala yote yanayohusiana na usafi na mazingira katika maeneo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

2. Kutoa ushauri kuhusu masuala ya tathmini na athari za usafi na mazingira.

3. Kupendekeza hatua stahiki za kuongeza ufanisi wa huduma za mitaro, michirizi na misingi ya maji ya mvua katika maeneo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

4. Kuandaa na kuwasilisha taarifa ya mifumo ya ardhi, majengo, mitaro na michirizi ya maji taka.

5. Kusimamia utekelezaji wa Kanuni za Usafi na Mazingira katika matumizi ya miundombinu ya mitaro, makaro, vyoo na michirizi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

6. Kushauri hatua za kuchukuliwa dhidi ya athari ya usafi na mazingira.

7. Kuandaa na kuwasilisha kwa Mkuu wa Idara makadirio ya gharama za mahitaji ya usafi na mazingira.

8. Kusimamia na kufatilia kazi maalum (operesheni) zinazohusiana na udhibiti wa mazingira na uendelezaji wa miji.

9. Kupendekeza maeneo ya utupaji na uhifadhi wa taka.

10. Kuandaa mikakati ya udhibiti wa mazingira, uhifadhi na uendelezaji wa miji.

11. Kuandaa na kupendekeza maeneo ya maegesho ya vyombo vya usafiri na vituo vya usafiri.

12. Kubuni, kupendekeza, kuanzishwa na kusimamia bustani na maeneo ya kupumzikia wananchi.

13. Kubuni, kupendekeza, kuanzishwa na kusimamia vyoo vya umma.

14. Kupendekeza na kusimamia utekelezaji wake Sheria ndogo ndogo, Kanuni, Miongozo na Matamko yanayohusiana na usafi na mazingira.

15. Kuandaa mpango wa taka ngumu na maji taka katika Mitaa.

16. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.

17. Kutoa ushauri kwa Mamlaka husika kuhusu masuala ya tathmini na athari za matengenezo ya miundombinu ya majengo, barabara, taa, alama na samani.

Divisheni hii itasimamia masuala ya mapato, uchumi na maendeleo ya Wajasiriamali ikiwa ni pamoja na kuwatambua na kuwawekea mazingira wezeshi kwa Wajasiriamali wadogo wadogo katika kutekeleza majukumu yao ya kufanya kazi.

Divisheni hii ina sehemu mbili (2) ambazo ni Sehemu ya Mapato na Sehemu ya Uchumi na Wajasiriamali.

Majukumu ya divisheni ya mapato uchumi na ujasiriamali

1. Kusanya ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

2. Kutoa taarifa za Mapato yanayokusanywa kutoka vyanzo mbali mbali vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

3. Kuandaa taarifa ya kila mwezi, robo mwaka, nusu na mwaka ya Mapato yote ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

4. Kufanya ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato katika maeneo ya makusanyo.

5. Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vyanzo vyote vya Mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

6. Kukagua maombi ya leseni za biashara.

7. Kuhifadhi Takwimu sahihi za Mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

8. Kulinda Usalama wa Mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

9. Kusimamia mapato kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo iliopo.

10. Kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

11. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.

12. Kufanya upembuzi wa mitaji ya wajasiriamali wadogo wadogo katika eneo
la Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

13. Kuandaa mfumo wa usajili wa wajasiriamali wadogo wadogo katika eneo la Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

14. Kusikiliza malalamiko na kero za wajasiriamali wadogo wadogo na kuzitafutia ufumbuzi.

15. Kuweka mazingira rafiki kwa wajasiriamali ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli zao; Kutoa elimu na kuwawezesha wajasiriamali.

16. Kutoa ushauri juu ya masuala yote yanayohusiana na Wajasiriamali.

17. Kufanya ukaguzi katika maeneo mbali mbali ya wajasiriamali kwa kuangalia utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo.

18. Kuwaunganisha wajasiriamali na taaissi za uwezeshaji wananchi kiuchumi.