Vitambulisho vya wajasiriamali

Vitambulisho vya wajasiriamali

Baraza la Manispaa ya Magharibi “A” linatoa huduma ya vitambulisho vya wajasiriamali kwa wafanya biashara wadogo wadogo ili kuwarahisishia katika upataji wa huduma kwa kufanya biashara zao bila kusumbuliwa na mamlaka husika.

Vitu vinavyohitajika ili kupata kitambulisho

1) Kitambulisho cha mzanzibari mkaazi, kitambulisho cha NIDA au leseni ya udereva.

2) Malipo ya  kiasi ya shilingi 30, 000 /= kila mwaka.

3) Ada ya usafi 15, 000 /= shilingi kwa mwezi.