Vibali vya ujennzi

Vibali vya ujenzi

Vibali vya ujenzi vipo vya aina mbili :-

1) Nyumba za kawaida garama yake ni kuanzia 150,000 /=  shilingi na kuendelea.

2) Nyumba za gorofa garama yake ni  kuanzia 1,000,000 /= shilingi  kwa kila gorofa moja.

Vitu vinavyohitajika ili kupata kibali cha ujenzi

  1. Fomu ya kibali cha ujenzi ada yake ni 20,000/= shilingi.
  2. Fomu ya sheha
  3. Kivuli cha hati miliki.
  4. Kivuli cha kitambulisho.
  5. Ramani ya mjengo.

Utaratibu wa vibali vya ujenzi

  1. Kufika katika ofisi ya mipango miji iliyopo katika ofisi ya Manispaa Magharibi "A"  kwa ajii ya kuchukuwa fomu. Kabla ya kuanza ujenzi.
  2. Kupeleka fomu kwa sheha wa shehia.
  3. Kurudisha fomu katika ofisi ya mipango miji.
  4. Ukaguzi wa eneo unaofanya na maasifa ya mipango miji.
  5. Kupatiwa kibali cha ujenzi.

Wanaostahiki kukata kibali cha ujenzi

  1. Watu wote wanaooanza kujenga katika eneo ya Manispaa ya Magharibi "A".
  2. Watu ambao vibali vyao vimeisha mda wake. Kumbuka kibali cha ujenzi ni mda wa mwaka mmoja.
  3. Watu waliojenga zamani kabla ya ukataji wa vibali na wanaendelea na ujenzi hivi sasa.