Mikopo ya asilimia kumi (10%)

Mikopo wa asilimia kumi (10%)

Ni mikopo inayotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kupatiwa wajasiriamali wadogo wadogo katika vikundi. Hasa imelenga kwenye makundi makuu matatu (3)  Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Sifa ya waombaji wa mikopo ya asilimia kumi (10%)

i. Wawe Wazanzibari wakaazi.

ii. Waombaji watoke kwenye makundi yaliyokusudiwa (Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu).

iii. Wawe kwenye vikundi vilivyo sajiliwa.

iv. Wawe na shughuli isiyopungua miezi ( 6 ) inayombewa mkopo tokea kuanzishwa kwake.

v. Wawe wakaazi kutoka Mamlaka ya Serikali za Mitaa husika.

vi. Wawe na utayari wa kupokea mafunzo kabla ya mkopo (Preloan training).

vii. Kikundi kisiwe na mkopo zaidi ya mmoja.

viii. Wakopaji wawe tayari kufungua Akaunti katika Benki husika. Ushiriki wa Wanachama wa kikundi uwe kwa asilimia (100%).

ix. Kikundi hakitajumuisha wajumbe wenye ajira rasmi.

x. Vikundi vyote view na idadi ya wanachama kwa mujibu wa sheria ya Ushirika pamoja na sheria Wakala wa Usajili wa Mali na Biashara (BPRA).

xi. Kikundi kisiwe na mchanganyiko wa wanakikundi kutoka makundi yote matatu yaliyotajwa (Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu).

xii. Kikundi kisipungue wanachama saba (7) na kuendelea.

Wanaostahiki kupatiwa mkopo ya asilimia kumi (10%)

Mfuko unalenga kutoa mikopo kwa makundi ya Vijana, Wanawake na Watu yenye Ulemavu kutoka katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, ambao watakuwa na sifa za kupatiwa mikopo kwa mujibu wa Muongozo huu. Sifa kubwa ni uwezo wa waombaji wawe wanaendelea kufanya shughuli za kiuchumi walizoomba mkopo, nao ni;

i. Watu walio katika makundi maalum (Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu)

ii. Wanawake kuanzia miaka 18 na kuendelea ambao wana shughuli za kiuchumi

iii. Vijana kuanzia miaka 18 hadi 35 kwa, wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi na wanahitaji kuendeleza shughuli zao

iv. Walengwa wote wawe na uzoefu usiopungua miezi 6 katika shughuli wanazozifanya, na;

v. Wawe wamesajiliwa rasmi katika taasisi zinazotambulika kisheria. (BPRA + Ushirika)

Kupoteza sifa kwa waombaji wa mkopo wa asilimia kumi (10%)

Kikundi kitahesabika kuwa kimepoteza sifa ya kupata mkopo endapo kitafanya yafuatayo:–

(a) Kitapoteza moja wapo ya sifa zilizainishwa katika kifungu namba 5.

(b) Hakijamaliza kurejesha mkopo uliotolewa na mifuko mingine.

(c) Kimetoa taarifa za uongo kwa wadau wanaosimamia mikopo (Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakala na Benki) kwa lengo la kujipatia fedha.

(d) Kimetumia fedha za mkopo kwa matumizi tofauti na yale yaliyoombewa mkopo bila ya idhini ya Wakala; au

(e) Kikundi kikiwa kina mchanganyiko wa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Shughuli za kiuchumi zinazoweza kuombewa mkopo wa asilimia kumi (10%)

i. Kilimo;

ii. Ufugaji;

iii. Kazi za mikono (Usarifu, Ufinyanzi, Uhunzi, Mafundi Seremala nk.) iv. Biashara ya huduma mfano utalii, Elimu, Afya, Usafiri na Mama/ Baba lishe na nyeginezo.

V. Miradi katika Sekta ya Mawasiliano (Mobile Money)

vi. Shughuli nyingine yoyote ya halali na yenye tija ya kuweza kulipia mkopo na wakopaji kuendelea kiuchumi.

ANGALIZO

Mfuko wa 4:4:2 hautahusika na maombi yeyote ya Boti za Uvuvi na Boti za Kilimo cha Mwani, kwa wanaohitaji Vifaa hivyo maombi yao yawasilishwe Wizara ya Uchumi wa Buluu.