Leseni ya biashara

Leseni ya biashara

Leseni ya biashara ni kibali cha kisheria kutoka serekalini au mamlaka husika kwa ajili ya shughuli za kibiashara au huduma za kitaalam.

Vigezo vya kupata Leseni za Biashara

i. Mfanyabiashara anapaswa awe na hati ya usajili iwapo anatumia jina la biashara (Certificate of Registration or Incorporation)

ii. Kama ni Kampuni mwombaji awe na “Memorandum of Article of Association” ambazo zinaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kufanya biashara anayoiomba.

iii. Awe na mahali/ Eneo linalokubalika kwa aina ya biashara anayoiomba na isiwe vibanda vilivyopo kando kando ya barabara.

iv. Mfanyabishara awe na kivuli cha Cheti cha namba ya mlipa kodi (TIN).

v. Masharti mengine ya kupata Leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha mfano Mkahawa inabidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake.

vi. Hati ya Utaalam (Professional Certificates) kwa biashara zote za kitaalamu.

Taratibu za kupata leseni za biashara

1. kufika ofisini kwa ajili ya kusajiliwa na kupatiwa leseni.

2. kufanyiwa ukaguzi ambao unafanywa na mtathmini wa biashara pamoja na Afisa wa Afya.

3. Kuwekewa kiwango cha bei kulingana na kanuni.

4. kufanya malipo kupitia PBZ Benki.

5. Kurejesha stakabadhi ya malipo ya Bank ofisini pamoja na viambatanisho vya leseni (picha ya passport size, kivuli cha kitambulisho).

6. Kufika ofisini kwa ajili ya kuchukuwa leseni.

Taratibu za kupata leseni za biashara kwa biashara za utaalam maalumu

1. Huduma za utaalam maalum ni kama; maabara, ukandarasi, uuzaji dawa, upuliziaji wa dawa ya kuua wadudu (fumigation), huduma za hospitali, maduka ya dawa, skuli, utaalam au ushauri n.k.

2. Mhusika ni lazima awe amesomea fani aliyoomba au kuajiri wataalam wenye sifa zinazotakiwa.

Taratibu

a)  Ujazaji wa fomu ya maombi ya leseni za biashara (Business license application form) kitengo cha mapato.

b) Ukaguzi wa maafisa mipango miji, afya na biashara. Ukaguzi huu unafanywa kwa baadhi ya biashara mfano bucha, Nyumba za kulala wageni, migahawa, mashine za kusaga, mashine za kukoboa na gereji.

c) Mfanyabiashara huandaliwa ( Control number ) kwa ajili ya malipo kulingana na biashara yake na anaenda kulipa kwa wakala au benki ya PBZ.

d) Muda wa leseni ni miezi 12, kuanzia Januari hadi Disemba mfanyabiashara anapewa miezi mitano ya kulipia leseni yake bila faini.

e) Utoaji wa huduma hizi mhusika anatakiwa awe amesajiliwa na mamlaka au bodi za uthibiti wa taaluma husika kama zilivyoorodheshwa.

Namba Huduma / Utaalam Mamlaka Husika
1 Ukandarasi wa ujenzi Zanzibar Contractors Registration Board (ZCRB)
2 Utengenezaji mahesabu / Ukaguzi wa hesabu Zanzibar Board of Auditors and Accountant (ZBAA)
3 Uwakili Zanzibar Law Society (ZLS)
4 Udaktari Zanzibar Medical Council (ZMC)
5 Uuzaji dawa, chakula na vipodozi Zanzibar Food and Drugs Authority (ZFDA)
6 Uuzaji wa dawa za binadamu Zanzibar Food and Drugs Authority (ZFDA)
7 Maduka ya gesi Certificate ya zimamoto

Malipo na Viwango mbalimbali vya ada vinavyotozwa ili kupata leseni za biashara.

Kiwango cha ada ya leseni kinatofautiana kulingana na aina ya biashara husika.Baada ya ulipaji wa ada hiyo mfanyabiashara atapatiwa stakabadhi kwa malipo halali ya fedha yake.

Wajibu wa mfanyabiasahra baada ya kupata leseni ya biashara.

 Kuhuisha/kulipia leseni kila mwaka mara moja tangu tarehe ilipotolewa kwa mujibu wa makadirio mpaka ukomo wa matumizi yake.

Mfanyabiashara anayehuisha leseni anatakiwa aje na nakala ya leseni iliyoisha muda wake.